Fomu za Kujiunga
- Home
- Fomu za Kujiunga
TAFADHALI SOMA MAELEZO KWA MAKINI
- Mtihani wa kujiunga na shule (Entrance & Interview) utafanyika SANTHOME SABS Girls’ Sec. School, NALA, DODOMA Tarehe 3 tofauti tofauti kama ifuatavyo;
- Tarehe 17 Septemba 2026, Alhamisi,
- Tarehe 19 Septemba 2026, Jumamosi na
- Tarehe 21 Septemba 2026, Jumatatu.
Siku zote mitihani tunaanza saa 2 kamili.
- Kadiri ya Muda wako chagua Tarehe. Ukisha chagua tarehe lazima uje siku hiyo hiyo kuandika mitihani.
- Urudi na fomu ya maombi siku ya mtihani. Fomu ya maombi iambatanishwe na Photo copy ya cheti cha Ubatizo na cheti cha Kuzaliwa.
- Fomu isiyo kamili haitapokelewa. Fomu ziwe original, photo copy haikubaliki. Picha ni lazima. Tumia mwandiko unao onekana vizuri kujaza.
- Kama ukichelewa kufika kwa wakati siku ya mtihani hutaruhusiwa kufanya mtihani.
- Uje na sare ya shule ya msingi uliyosoma siku ya mtihani.
- Wanafunzi waliomaliza darasa la saba tu wanastahili kuja kufanya mtihani wetu.
- Kufaulu mtihani wa Taifa wa darasa la 7 ni muhimu ili kupata nafasi katika shule ya Sekondari.
- Majina ya wanafunzi watakao faulu yatatangazwa tarehe 22 SEPTEMBA 2026 hapa shuleni saa 3.00 asubuhi, na waliofaulu watajulishwa kwa njia ya SIMU. Pia itapostiwa katika website ya shule.
- Kalamu moja inatosha siku ya mtihani.
- Tutakuwa na mitihani miwili, mmoja mchanganyiko na mmoja Hisabati peke yake, pia wote watahojiwa (personal interview).
- Siku ya mtihani, saa nane tutakuwa tumemaliza shughuli zote.
- Wanafunzi watakaopata ALAMA za JUU, ndiyo watakao chaguliwa. Maamuzi ya shule ndiyo ya mwisho katika swala hili.
- Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 19/09/2026 siku ya Jumatano.
- Pre Form One in mwezi miwili kuanzia 03/10/2026 hadi 03/12/2026. Gharama itakuwa 600,000/=. Watakao faulu Pre Form One vizuri ndiyo wana ingia Form One.
- Mtoto mwenye matatizo ya tumbo (Ulcers) au ugonjwa nyingine inayo takiwa kuhudumiwa kwa karibu asije kwenye shule hii ya Bweni. Kwa vile hatutoi chakula cha pekeee. Magonjwa mengine kama asthma, kifafa n. k. hayafai katika Shule ya Bweni.
- Kwa wale wanafunzi ambao wanatoka nje ya Wilaya ya Dodoma ni LAZIMA na vema wawe na mlezi mwenyeji wa hapa Dodoma aliye tayari kufika hapa shuleni wakati wowote anapohitajika
Comments are closed.