Mfumo wa maombi umefungwa kwasababu muda wa kupokea maombi ya kujiunga na shule umekwisha. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Tafadhali usifanye malipo na ikiwa umefanya malipo rudisha muamala.
Jinsi ya kujiunga na shule yetu
Tafadhali bofya hapa kusoma maelezo ya kina kabla ya kulipia fomu
Maelekezo ya kununua fomu mtandaoni
- Lipia TSh 25,000/= kwenye mojawapo ya namba zifuatazo
 |
0764 637 877 Jina: SANHTOME SABS GSS |
Tumia namba ya simu kufanya malipo. Usiweke pesa kwa wakala wala kuhamisha toka benki kuja kwetu moja kwa moja.
Ukitumia wakala / benki hatutapata namba ya simu iliyofanya malipo hivyo mifumo yetu haitaweza kushughulikia muamala wako
-
Ndani ya muda mfupi tutakutumia ujumbe kwenye namba uliyoitumia kufanya malipo. Ujumbe huo utakuwa na token.
-
Bonyeza Pakua fomu. Ingiza namba ya simu uliyotumia kufanya malipo.
-
Ingiza token tuliyokutumia kwa ujumbe mfupi
-
Ingiza majina mawili ya mwanafunzi kwenye sehemu husika, kama alivyosajiliwa kwenye mtihani wa darasa la saba. Ingiza pia eneo anakotokea
-
Ingiza jina la shule aliyomaliza darasa la saba. Kisha chagua kama ni English Medium au shule ya Kiswahili.
-
Chagua tarehe atakayoweza kufika shuleni Dodoma saa mbili asubuhi kufanya interview kati ya siku tatu zilizoorodheshwa. Hakutakuwa na interview nyingine
-
Hakiki taarifa hizi kwani hutaweza kubadilisha, kisha bonyeza Hifadhi Taarifa
-
Pakua fomu. Ichape na ufuate maelekezo yake.
-
Siku ya interview uliyochagua, uje na fomu original iliyoambatanishwa picha pamoja na vyeti vya mwanafunzi shuleni Dodoma.